• Latest News

    Friday, 2 March 2018

    SIMBA SC YATOKA SARE DHIDI YA STAMD UNITED 3-3

    Leo march 2 ,2018 Simba imeshindwa kupata ushindi kwa Stand United baada ya kulazimishwa sare ya kufungana 3-3 kwenye mchezo wa ligii kuu uliochezwa uwanja wa taifa.
    Asante Kwasi alifunga bao la kwanza katika mchezo huo, Laudit Mavugo akafunga goli la pili na kuondoa ukame wa kutofunga aliodumu nao kwa muda mrefu. Stand United wakiwa chini kwa tofauti ya goli 2-0 wakapambana na kusawazisha magoli yote kabla ya kwenda mapumziko, magoli yao yalifungwa na Tariq Seif pamoja na Aron Lulambo.

    Simba wakafunga goli la tatu kupitia kwa Nicholas Gyan lakini muda mfupi baafaye Birigimana Blaise akaisawazishia Stand United na kufanya matokeo kuwa 3-3.

    Sare ya leo inaifanya Simba ifikishe pointi 46 na kuendelea kuongoza kwenye msimamo ligi baada ya kucheza mechi 20 huku wakifuatiwa na Yanga ambao wana pointi 40 katika nafasi ya pili lakini wao wamecheza mechi 19.

    No comments:

    Post a Comment