Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo February 28,2018 amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu kutowafungia ndani na badala yake wawapeleke shule.
Kassim Majaliwa amesema ulemavu si kigezo cha kuwakosesha watoto hao kupata elimu na kufanya kazi, hivyo amewataka jamii kutowakatisha tamaa na kuaapeleka mashuleni.
Waziri mkuu ametoa agizo hilo wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa majengo ya chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala mkoani Mtwara .

No comments:
Post a Comment