Club ya Man City inayofundishwa na kocha Pep Guardiola usiku wa February 25 2018 ilifanikiwa kutwaa taji lake la kwanza msimu wa 2017/2018 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Wembley jijini London , mchezo huo ulikuwa mchezo wa fainali ya Carabao Cup.
Guardiola amefanikiwa kuiongoza Man City dhidi ya Arsenal kupata ushindi wa magoli 3 kwa 0, magoli ya Man City yalifungwa na Sergio Aguero dakika ya 18 Vincent Kompany dakika ya 58 na goli la mwisho likafungwa na David Silva dakika ya 65.
Kutwaa taji hilo kwa Man City kunawafanya wafikishe jumla ya mataji matano ya Kombe la Ligi.



No comments:
Post a Comment